Mwenyekiti wa Shirikisho la Wakuu wa Majeshi ya Polisi Ukanda wa Kusini mwa Afrika (SARPCCO), IGP Camillus Wambura, leo Septemba 30, 2024 amefanya mazungumzo na ujumbe kutoka Sekretarieti ya SARPCCO na SADC Ofisi ya Harare Zimbabwe.
Wajumbe wa Sekretarieti hiyo wamefanya ziara hiyo kwa lengo la kumpitisha Mwenyekiti wa SARPCCO katika Majukumu atakayoyasimamia katika kipindi chake Cha Uenyekiti ikiwemo Usimamizi wa Operesheni mbalimbali za Uhalifu unaovuka mipaka.
Ujumbe huo unaongozwa na Afisa Mwandamizi Kitengo Cha Polisi, Sekretarieti ya SADC/SARPCCO Bi Thanyani Gumede na Mkuu wa INTERPOL (Regional Bureau – RB) Harare Sello Moerane
IGP Wambura alikabidhiwa Uenyekiti huo Juni 13, 2024 na ataongoza Shirikisho hilo kwa kipindi cha mwaka mmoja.