Nidhamu Haki Weledi na Uadilifu ni msingi wa mafanikio Yetu.

zawadi2

Polisi kata wapongezwa, waliofanya vizuri 2023 wapewa vyeo na Waziri Massauni.

Serikali imesema itaendelea na mpango wake wa kuhakikisha Jeshi la Polisi linakwenda zaidi kwa Wananchi hadi ngazi ya Kata kwa kuwatumia Polisi Kata ili kuzuia uhalifu na kuendelea kutoa huduma bora kwa Wananchi.

Kauli hiyo imetolewa na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Massauni wakati wa Sherehe za kuwapa sifa na zawadi Watumishi wa Wizara hiyo waliofanya vizuri kwa mwaka 2023, Sherehe zilizohudhuriwa na Viongozi mbalimbali na Askari kutoka Vyombo vya Usalama vilivyo chini ya Wizara hiyo.

Kwa upande wake Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Camillus Wambura akizungumza kwa niaba ya Wakuu wa Vyombo vya Usalama vilivyopo chini ya Wizara hiyo amesema Watumishi ndani ya Wizara hiyo wana deni kubwa la kulipa kwa Serikali kutokana na uwezeshaji ambao umekuwa ukifanyika wa kuboresha mazingira ya kufanyia kazi.

Katika Sherehe hizo Askari mbalimbali wa Wizara hiyo walizawadiwa wakiwemo Polisi Kata ambao waliweza kupandishwa vyeo ili kuhamasisha wengine kufanya vizuri zaidi katika kuipeleka dhana ya Polisi Jamii kwa Wananchi.

Polisi Kata hao waliopandishwa vyeo na kupewa zawadi ya pikipiki na fedha taslimu Shilingi Milioni Moja ni kutoka Kata ya Biro Morogoro, Mabatini Mwanza, Mkunwa Mtwara, Shehia ya Uzi Zanzibar na Mkuu wa Dawati la Jinsia na Watoto Polisi Mkoa wa Katavi.

 

Related news