UN JOBS

Tangazo la kazi umoja wa mataifa – MONUSCO

Umoja wa mataifa kupitia idara ya ulinzi wa amani (DPO) wametangaza nafasi ya kazi misheni ya ulinzi wa amani umoja wa mataifa nchini jamhuri ya kidemokrasia ya congo (monusco) kwa maafisa wa polisi wenye sifa kama ifuatavyo: –
1. Deputy police commissioner, p-5 (2023-MONUSCO-49448- DPO)
sifa za jumla za waombaji ni: – shahada ya uzamili katika fani zifuatazo: – sheria, menejimenti ya polisi, usimamizi wa sheria, haki jinai, masomo ya usalama, utawala, rasilimali watu, sayansi ya jamii, na masomo ya usalama, kwa wenye shahada za fani tajwa hapo juu wawe na sifa za uzoefu katika usimamizi wa sheria, utawala wa polisi na ulinzi wa amani.
Awe na uzoefu wa miaka 15 katika kazi za polisi, usimamizi wa sheria za nchi au za kimataifa, awe na uzoefu wa kutunga sera, usimamizi wa fedha, mipango ya kimkakati, kuongoza kamandi na kufanya kazi makao makuu ya polisi. Aidha, awe na cheo kuanzia mrakibu wa polisi na kuendelea.  Pia awe na uwezo wa kuongea na kuandika lugha ya kiingereza na kifaransa.

Inashauriwa nafasi hii iombwe na maafisa wenye sifa na
uzoefu wa operesheni za ulinzi wa amani na waliowahi
kuomba siku za nyuma.
Waombaji wote wajaze fomu za maombi EAC (Employment and Academic Certification na P.11(personal history) zinazopatikana kwenye tovuti ya Polisi https://polisi.go.tz/publications/   na zitumwe kwenye barua pepe: co.ir@tpf.go.tz. Jazeni fomu hizo kwa umakini kulingana na maelekezo husika. Mwisho wa kuwasilisha fomu za maombi ni tarehe 19 julai, 2024.

Fomu zitakazowasilishwa baada ya muda ulioelekezwa katika tangazo hili hazitafanyiwa kazi

kutoka: kitengo cha uhusiano wa kimataifa – PHQ DODOMA

Related news